Kenya yachagua kikosi cha kuteka dunia mbio za nyika

MABINGWA mara 23 wa dunia Kenya wamechagua kikosi cha kudondosha mate kwa makala ya 45 ya Mbio za Nyika za Dunia zitakazofanyika jijini Belgrade, Serbia mnamo Machi 30, 2024.

Agnes Ngetich, Emmaculate Anyango na Lilian Kasait wanaokamata nafasi tatu za kwanza kwa muda bora duniani mwaka huu katika mbio za kilomita 10 za barabarani wa dakika 28:46, 28:57 na 29:32, mtawalia, wako katika kikosi cha taifa cha wakimbiaji 30 kilichochaguliwa katika uwanja wa Chuo cha Mafunzo cha Magereza mjini Ruiru, Kiambu, Jumamosi.

Beatrice Chebet na Ngetich waliozoa dhahabu na shaba mtawalia kwenye Mbio za Nyika za Dunia 2023 nchini Australia, bingwa wa 21km kwenye Riadha za Dunia za Barabarani 2023 Margaret Chelimo pamoja na mshindi wa mbio za nyika za majeshi Cintia Chepngeno wanakamilisha orodha ya washiriki sita watakaotimka kitengo cha 10km cha wanawake. Chepngeno alikosa kumaliza mbio nchini Australia kwa hivyo amepata fursa nzuri ya kujifariji.

Bingwa wa dunia 21km kwenye Riadha za Dunia za Barabarani 2023 Sebastian Sawe ataongoza kikosi cha 10km wanaume kilicho na mfalme wa mbio za nyika kitaifa 2022 Samuel Chebolei, bingwa wa dunia mara mbili mbio za nyika Geoffrey Kamworor pamoja na Gideon Rono, Benson Kiplagat na bingwa wa dunia kitengo cha chipukizi 2023 Ishmael Kipkurui.

“Nilikuwa na matumaini makubwa ya kutwaa tiketi. Mpango wangu wa kutoonekana na kuchomoka zikisalia mita 500 naona ulifanya kazi vizuri,” akasema Sawe anayelenga medali jijini Belgrade.

Reynold Cheruiyot aliyemaliza nyuma ya Kipkurui pamoja na washindi wa dhahabu ya mbio mseto Emmanuel Wanyonyi na Kyumbe Munguti, sawa na Diana Chepkemoi, Emmanuel Wanyonyi na Charles Rotich watapata fursa ya kuimarisha matokeo yao kutoka mwaka 2023.

Timu ya chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 ya Kenya inajumuisha Sheila Chebet, Deborah Chemutai, Nancy Cherop, Mercy Chepkemoi, Diana Cherotich na Diana Chepkemoi (wanawake kilomita sita) na Samuel Kibathi, Charles Rotich, Mathew Kipkoech, Jonah Erot, Shadrack Rono na Gideon Kipngetich (wanaume kilomita nane).

Cheruiyot, Wanyonyi, Munguti, Virginia Nyambura, Mercy Wanjiru na Purity Chepkirui watashiriki mbio mseto.

Connexion utilisateur

Commentaires récents

  • Compère-lapinisme linguistique en l'île aux fleurs fanées

    Albè, sans vouloir aller vers une...

    Frédéric C.

    18/09/2025 - 15:05

    ...indépendance à la mauricienne ou la barbadienne, c’est précisément les "révolutionnaires" dont Lire la suite

  • Compère-lapinisme linguistique en l'île aux fleurs fanées

    SORTIR DE LA TRAPPE

    Albè

    18/09/2025 - 11:52

    Très simple : une indépendance à la barbadienne ou à la mauricienne. Lire la suite

  • Compère-lapinisme linguistique en l'île aux fleurs fanées

    Hélas, Fondas...

    Frédéric C.

    18/09/2025 - 11:07

    ...en effet, ce konpèlapinisme-ci, comme d’autres tout aussi "malsains", est qqch qui imprègne bp Lire la suite

  • Visite officielle du président du Tchad, Mohamed Idris Itno, en Algérie

    Albè, je ne parle pas...

    Frédéric C.

    18/09/2025 - 02:40

    ...de la Mque ni du PPM, mais de l’Algérie à l’époque où Fanon y militait pour sa libération nati Lire la suite

  • Algérie : Mustapha Hidaoui nommé Ministre de la Jeunesse

    DELIRES...

    Albè

    17/09/2025 - 13:17

    Arrêtez vos délires anti-musulmans ! Lire la suite